Mwanzo

Kutoka Swahilinux Wiki
Pitio kulingana na tarehe 18:19, 19 Mei 2020 na Admin (Majadiliano | michango)
Jump to navigation Jump to search

Swahilinux Microsystems.

Swahilinux Microsystems ni kampuni iliyosajiliwa nchini Kenya na inayotambulika kwa kuwa ya kwanza ya kutengeneza Mfumo wa Tarakilisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Mfumo huo wenye jina Tembo GNU/Linux, ndio mradi mkubwa kuwahi kufanywa na Swahilinux na ulitolewa mwezi wa Desemba mwaka wa 2019. Hii ni miezi sita baada ya Swahilinux kuanzishwa.

Lengo kuu la Swahilinux ni kufanya utafiti na kutengeneza suluhisho kwa matatizo yanayokumba Afrika kwa ujumla. Kila uchao Swahilinux inazidi kukua, kutambua na kutengeneza suluhisho mpya. Swahilinux inatumia leseni wazi kwa miradi nyingi zake na mfumo wazi wa uvumbuzi ili kukuza talanta na kuwezesha watu wenye asili za kiafrika kutengeneza suluhisho kwa matatizo yanayokumba waafrika.