Mwanzo

Kutoka Swahilinux Wiki
Jump to navigation Jump to search

Swahilinux Inc. ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa ya Kenya yenye makao makuu jijini Nairobi. Inakuza, inazalisha, inatoa leseni, inasaidia, na inauza programu za kompyuta, kompyuta za kibinafsi, na huduma zinazohusiana. Inakusudia kuwa mmoja wa watoaji wakubwa wa huduma za kiteknolojia kwa watu wa Kiafrika na huchangia sana katika teknolojia ya mfumo wazi.

Mradi unaojulikana zaidi wa Swahilinux Inc. ni mradi wa Tembo GNU/Linux ambao unazingatia ujanibishaji wa teknolojia kwa lugha za Kiafrika huku lugha ya Kiswahili ikifanywa kuwa ya hali msingi. Tembo GNU/Linux bado iko katika hali ya uvumbuzi na toleo la kwanza la aina ya beta ilifanywa mnamo tarehe 31 Desemba 2020.

Swahilinux Inc. ilianzishwa na Jeremiah Rotich & Kevin Obuya kama mradi mmoja yenye madhumuni ya kuunda mfumo wa uendeshaji wa Kiswahili ambao baadaye ulibadilishwa na hamu ya kutengeneza suluhisho zinazolenga kutatua shida na changamoto za bara Afrika.